Miche zaidi ya 1,000+ ya pandwa kuadhimisha siku ya Misitu Duniani

 Green Awareness Club Tanzania, kama Klabu ya Mazingira yenye Matawi mengi zaidi Tanzania imetumia Siku ya Misitu Duniani (21.03.2023) kupanda Miche ya Miti kwenye Mashule mbalimbali Nchini. Ambapo tumeweza kupanda Miche ya Miti kwenye Shule 7 na Mikoa 7 tofauti Tanzania na kufikisha jumla ya Miche zaidi ya 1,000 iliyo pandwa ikiendana na Uelimishaji kuhusu umuhimu wa Utunzaji wa Misitu na Mazingira Kwa afya zetu.


Aidha Mwenyekiti Taifa wa Green Awareness Club, ame washukuru Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kwa ushirikiano wao Mkubwa wa kuwapatia Miche hiyo pamoja na utaalamu, pia Chuo Cha Misitu Olmotonyi (FTI), Halmashauri za wilaya na Mikoa pamoja na Vyombo vya habari walio ungana nasi.


Ifuatayo ni Matukio mbalimbali ya upandaji Miti, mikoa mbalimbali Nchini.

DAR ES SALAAM

Tukio lilifanyika Shule ya sekondari Mabibo na Shule ya Msingi makuburi. 

Ambapo tulipanda Miche ya Miti 150.





PWANI
Tukio lilifanyika Shule ya sekondari Mwinyi, ambapo tulipanda Miche ya Miti 100.





ARUSHA 

Tukio lilifanyika Shule ya Msingi Ngorbob iliyopo Kisongo, Arusha. Miche 120 ilipandwa.








KILIMANJARO 

Tukio lilifanyika Shule ya Msingi Kivulini, wilaya ya Mwanga, Kilimanjaro. Miche 150 ilipandwa.





GEITA 

Tukio lilifanyika Shule ya Msingi Ibondo iliyopo wilaya ya Chato, Geita. Miche 300 ilipandwa.





DODOMA 

Tukio lilifanyika Shule ya Msingi NG'ONG'ONA, ambapo Miche ya Miti 150 ilipandwa.






MBEYA
Tukio lilifanyika Shule ya Msingi Pambogo, ambapo Miche 150 ilipandwa.






Shukrani za dhati ziwaendee wote walio shiriki zoezi hili.