Green Awareness Club kupanda Miti Tanzania nzima
Katika kuelekea siku ya Misitu Duniani (21.03.2023), Green Awareness Club
Kama Klabu ya Mazingira inayojihusisha na Uelimishaji na uhamasishaji jamii kutunza Misitu na Mazingira.
Tumepanga kutumia siku hiyo kupanda Miche ya Miti na kutoa elimu kwa Wanafunzi juu ya utunzaji wa Misitu kwenye Shule mbalimbali za Msingi na sekondari, kwenye Mikoa mbalimbali hapa Nchini (Tanzania).
Ambayo ni Dar es salaam, Arusha, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro, Pwani, Kigoma.
Tuna wakaribisha WanaMazingira na Wadau mbalimbali kuungana nasi kwenye siku hii muhimu Kwa WanaMazingira Duniani.
Karibu tuungane kuhamasisha utunzaji Misitu na Mazingira:-
Barua pepe: greenawarenesstz@gmail.com
Simu: +255689217500